WIMBO
Yesu mpenzi nakuabudu, Msalabani unapohangaika, Nchi yatetemeka kwa hofu Na jua, na jua linafifia.
KITUO CHA KUMI NA MBILI.
Yesu anakufa msalabani.
Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.
Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba mtakatifu.
Ee Yesu uliyekufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu, unijalie niichukie dhambi, nisiishi kamwe katika dhambi.
Nifahamu kwamba nilipobatizwa kwa jina lako, nilibatizwa katika mauti yako, ili utu wangu wa kale usulibishwe nawe, mwili wa dhambi uangamizwe, nisitumikie tena dhambi.
Baba yetu…(×1)
Salamu Maria…(×1)
Atukuzwe Baba na..(×1)
K.Ee Bwana, utuhurumie……
W.Utuhurumie…
Roho za waamini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani.
Amina.
0 Comments