WIMBO
Pamoja nawe kaburini, Zika dhambi na ubaya wa moyo, Yesu tuwe Wakristo kweli Twakupa, twakupa saaa mapendo.
KITUO CHA KUMI NA NNE.
Yesu anazikwa kaburini.
Ee Yesu tunakuabudu tunakushukuru.
Kwa kua umewakomboa watu kwa Msalaba wako Mtakatifu.
Ee Yesu, ulizikwa kaburini, ukafufuka siku ya tatu.
Mimi pia nilizikwa pamoja nawe kwa njia ya ubatizo katika mauti yako.
Kwa vile wewe ulifufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, unijalie nami nifufuke, yaani nishike mwenendo mpya, mwenendo wa uzima wa neema.
Baba yetu…(×1)
Salamu Maria…(×1)
Atukuzwe Baba na…(×1)
K.Ee Bwana, utuhurumie…..
W.Utuhurumie….
Roho za waamini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani.
Amina.
Wimbo
Katika roho yangu Bwana Chora mateso niliyokutesa Nisiyasahau madeni Na kazi na kazi ya kuokoka.
Mbele ya altare:
Yesu wangu, kwa uchungu wote uloona juu ya msalaba na kwa kuzimia kwako kwa ukali wa mateso, unijalie nguvu ya kuvumilia kwa moyo taabu zote sasa na saa ya kuzimia kwangu.
Nawe Maria Mamangu.
Kwa uchungu wote ambao moyo wako umejaa ulipomnwona Mwanao mpenzi kuinama kichwa na kuzimia, unifadhili nife kifo chema.
Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.
Amina.
0 Comments