Mje Malaika wa mbingu, Funikeni mwiliwe kwa huruma, Vidonda vyake na utupu Askari, askari wamemvua.
KITUO CHA KUMI.
Yesu anavuliwa nguo.
Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.
Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba mtakatifu.
Askari wanamvua kwa nguvu nguo yake, iliyogandamana na madonda yake; wanayaamsha mara moja mateso yote aliyoteswa tangu mwanzo.
Ee Yesu, unayavumilia mateso makali haya, upate kunifundisha kuuvua kwa nguvu moyoni mwangu urafiki mbaya au kitu kingine chochote kile kinachoharibu urafiki wa Mungu, hata ikinipasa kutoa sadaka kubwa.
Baba yetu…(×1)
Salamu Maria…(×1)
Atukuzwe Baba na…(×1)
K.Ee Bwana, utuhurumie…
W.Utuhurumie…
Roho za waamini wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa amani.
Amina.
0 Comments