WIMBO
Mwokozi sasa ni ya tatu Waanguka chini ya msalaba. Katika dhambi za uregevu Nijue, nijue kutubu hima.
KITUO CHA TISA.
Yesu anaanguka mara tatu.
Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.
Kwa kuwa umewakomboa with kwa msalaba wako mtakatifu.
Ee Yesu unayezidi kudhoofika kwa mateso unaanguka mara ya tatu, upate Kunistahilia neema ya kuutiisha mwili Wangu na kuusulibisha, licha ya kuepuka nafasi za dhambi.
Mara ngingi mno ninajibovusha kwa kupenda mno starehe na tafrija.
Ee Yes mwema, nisaidie kuufuata mfano wa Mtakatifu Paulo, niutese mwili wangu na kuutumikisha, ili nipate siku moja tuzo mbinguni.
Baba yetu…(×1)
Salamu Maria…(×1)
Atukuzwe Baba na..(×1)
K.Ee Bwana, utuhumie….
W.Utuhurumie….
Roho za waamini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani.
Amina.
0 Comments