Ole mslaba huo mzito, Apagazwa mwana mpenzi wa Mungu.
Mwiliwe waenea mateso.
Alipa, alipa madhambi yetu.
.KITUO CHA PILI.
Yes anapokea msalaba
Ee Yesu, tunakuabudu, tunakushuru.
Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba mtakatifu.
Yesu anakubali kuelemewa na msalaba kwa ajili ya wokovu wa watu. Ndivyo anavyonifundisha moyo wa sadaka, moyo wa kujitolea na kujisahau kwa ajili ya wenhine.
Ee Yesu wangu mkarimu, mimi pia ninao msalaba wangu; jirani zangu, mwezangu wa ndoa, watoto, wazazi wangu, kazi zangu, joto, baridi, njaa, kiu, vishawishi, magonjwa na matatizo mengine ya maisha, wajibu wangu kwa Mungu, kwa Umma na kwa Kanisa, hayo yote in msalaba.
Unipe ukarimu wako ee Yesu, niyapokee bila ya kunung’unika, na kuyabeba vema.
Baba yetu…(×1)
Salamu Maria….(×1)
Atukizwe Baba na…(×1)
K.Ee Bwana, Utuhurumie…..
W.Utuhurumie…..
Roho za waamini wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani.
Amina.
0 Comments