Ad Code

𝗙𝗔𝗛𝗔𝗠𝗨 𝗨𝗧𝗢𝗙𝗔𝗨𝗧𝗜 𝗞𝗔𝗧𝗜 𝗬𝗔 𝗣𝗘𝗧𝗘 𝗬𝗔 𝗔𝗦𝗞𝗢𝗙𝗨 𝗡𝗔 𝗜𝗟𝗘 𝗬𝗔 𝗣𝗔𝗣𝗔.

Najua wengi wanajiuliza ni kwanini, Askofu au Papa huvaa pete wakati hajafunga ndoa? Je pete hizo humaanisha nini na kwanini wanazivaa?

Jibu rahisi ni kwamba, pete ni kielelezo cha mamlaka ya Kiaskofu au Mchungaji mkuu wa Jimbo. Kwahiyo pete anayovaa Askofu au Papa, sio sawa na zile wanazovaa wanandoa. Kwani pete hizi huwa zina maana kubwa sana ndani ya Kanisa na yule anayevaa.

Kiufupi niseme tu kuwa, kwa wanandoa pete ni ishara inayoashiria upendo na uaminifu wao juu ya agano hilo takatifu wanalofunga, lakini kwa Askofu pete imepewa hadhi kubwa sana ya Jimbo. Hivyo Askofu anapovaa pete humkumbusha kuwa, hata yeye ana wajibu wa kulipenda Kanisa na kulitumikia kwa moyo wake wote, kama ilivyo kwa wanandoa katika familia zao.

𝗦𝘄𝗮𝗹𝗶: 𝗦𝗮𝘀𝗮 𝘂𝘁𝗼𝗳𝗮𝘂𝘁𝗶 𝗸𝗮𝘁𝗶 𝘆𝗮 𝗽𝗲𝘁𝗲 𝘆𝗮 𝗔𝘀𝗸𝗼𝗳𝘂 𝗻𝗮 𝗶𝗹𝗲 𝘆𝗮 𝗣𝗮𝗽𝗮 𝗻𝗶 𝗶𝗽𝗶?

𝗝𝗶𝗯𝘂: Ukweli ni kwamba, Maaskofu wote huvaa pete, na pete hizi huwa na majina tofauti tofauti za kingereza.

1. 𝗙𝗜𝗦𝗛𝗘𝗥𝗠𝗘𝗡'𝗦 𝗥𝗜𝗡𝗚

Hii ni aina ya pete anayovaa Papa, ambayo hujulikana kama "PETE YA MVUVI". Mara nyingi hutengenezwa kwa dhahabu na kuchorwa picha ya Mtakatifu Petro katikati yake akiwa ndani ya mashua, huku pembeni kidogo mwa hiyo picha panaandikwa jina la Papa aliyeko kwenye kiti hicho kwa sasa.

Pete hiyo ya mvuvi limepewa jina hilo, hasa baada ya Yesu kumwambia Petri: " Njoo na unifuate, nami nitakufanya uwe mvuvi wa watu". (Luka 5:10).

Kwahiyo Papa akishateuliwa, huchagua jina jipya kama ishara ya kuitwa kwake katika kazi hiyo kuu ya kiuchungaji na kupewa pete hii. Lakini anapokufa, basi pete hii nayo huaribiwa, maana ilikuwa ni agano lake binafsi na Mungu katika kuliongoza Kanisa.

2. 𝗘𝗣𝗜𝗦𝗖𝗢𝗣𝗔𝗟 𝗥𝗜𝗡𝗚

Hii ni pete anayovaa Askofu katika mkono wake wa kulia, kidole cha tatu kutoka dole gumba kama anavyovaa Papa, wala haina utofauti katika uvaaji wake.

Lakini pete hii mara nyingi huonesha muungano wa ndoa uliopo katika Kristo na Kanisa lake. Hivyo kwa kuwa Askofu humwakilisha Kristo kama Kuhani mkuu, basi naye ana wajibu wa kulipenda Kanisa na kulitumika siku zote kama Yesu alivyofanya hata ikibidi kutoa uhai wake. (Waefeso 5:25).

Kwahiyo pete hii kwa Askofu nayo huwakilisha mamlaka aliyonayo katika Kanisa, na Mara zote huwa ni kubwa na za dhahabu. Lakini muundo wake ni wa tofauti tofauti sana, na siku zote hurithishwa kutoka kwa Askofu mmoja kwenda kwa mwengine baada ya Askofu aliye madaraka kufa, maana ni mali ya Kanisa.

Mwisho niseme pia, hata Makardinali na Maabate nao huvaa pete na pete zao huwa zina hadhi ya Kiaskofu, lakini zenyewe hutengenezwa kwa mapendekezo ya Baba Mtakatifu.

𝗧𝗨𝗠𝗦𝗜𝗙𝗨 𝗬𝗘𝗦𝗨 𝗞𝗥𝗜𝗦𝗧𝗢...

Post a Comment

0 Comments