Ad Code

HESBL || MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO | DIPLOMA

1.0       UTANGULIZI

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuujulisha umma kuwa upangaji wa mikopo ya Stashahada (Diploma) kwa mara ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2023/2024 umekamilika na imetuma orodha ya wanafunzi waliodahiliwa katika vyuo 36 kwa ajili ya kukamilisha taratibu za malipo.

HESLB itaanza kupeleka fedha kwa wanafunzi waliopangiwa mikopo katika vyuo husika siku chache zijazo na wanafunzi walioomba mikopo katika ngazi ya stashahada wanashauriwa kupata taarifa za kina kupitia akaunti walizozitumia kuomba mkopo maarufu kama SIPA (Student’s Individual Permanent Account).

BOFYA HAPA KUINGIA KATIKA ACCOUNT ILI KUTAZAMA JINA LAKO

2.0       UTARATIBU WA MALIPO

Utaratibu wa malipo kwa wanafunzi wa Stashahada waliopangiwa mikopo unaendelea na Maafisa wa HESLB wameanza kwenda katika vyuo husika ili kushirikiana na uongozi wa vyuo hivyo kupokea taarifa muhimu za wanafunzi zikiwamo za Benki na namba za usajili vyuoni.

3.0       MIKOPO YA STASHAHADA 2023/2024

Mikopo ya ngazi ya Stashahada imetolewa kwa mara ya kwanza mwaka huu wa masomo 2023/2024 kwa wanafunzi waliodahiliwa katika fani sita za kipaumbele zifuatazo:

       i. ‘Health & Allied Sciences’;

       ii. ‘Education and Teaching’;

       iii. ‘Transport & Logistics’;

       iv. ‘Energy Engineering’;

       v. ‘Mining & Earth Science’ &

       vi. ‘Agriculture & livestock





4.0       HITIMISHO

HESLB inawashauri wanafunzi ambao wana sifa na ambao hawakuomba mikopo ndani ya muda uliokuwa umetolewa awali (tarehe 07 Oktoba, 2023 hadi tarehe 30 Oktoba, 2023), wafike kwa uongozi wa vyuo walikodahiliwa au wapige simu 0736 665 533 au watume barua pepe info@heslb.go.tz au watume ujumbe kwa WhatsApp 0739 665 533 ili kupata ufafanuzi.

Post a Comment

0 Comments