Ad Code

MASOMO YA MISA DESEMBA 1, 2023 IJUMAA , JUMA LA 34 LA MWAKA




SOMO 1
Dan. 7:2-14

Danieli alinena akisema, Naliona katika maneno yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nane za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa. Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali. Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu. Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tena.

Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vine; akapewa mamlaka. Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wanne, mwenye kutisha, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipange vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe nne. 

Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na mbacho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.

Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.

Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe; nalitazama hata mnyama yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto. Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyang’anywa mamlaka yao; walakini maisha yao yalidumishwa kwa wakati na majira. Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.

Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo haitapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.


WIMBO WA KATIKATI
Dan. 3:75-81 (K) 59

(K) Msifuni na kumwadhimisha milele.

Milima na vilima, mhimidini Bwana;
Msifuni na kumwadhimisha milele.
Mimea yote ya nchi, mhimidini Bwana;
Msifuni na kumwadhimisha milele. (K)

Chemchemi, mhimidini Bwana;
Msifuni na kumwadhimisha milele.
Bahari na mito, mhimidini Bwana; 
Msifuni na kumwadhimisha milele. (K)

Nyangumi na vyote viendavyo majini, 
Mhimidini Bwana;
Msifuni na kumwadhimisha milele.
Ndege zote za angani, mhimidini Bwana;
Msifuni na kumwadhimisha milele.
Hayawani na wanyama wafugwao, mhimidini Bwana;
Msifuni na kumwadhimisha milele. (K)


SHANGILIO

Aleluya, aleluya,
Unifahamishe nami nitaishika sheria yako 
nitaitii kwa moyo wangu wote.
Aleluya.


INJILI
Lk. 21:29-33

Yesu aliwaambia wanafunzi wake mfano, Utazameni mtini na miti mingine yote. Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu. Nanyi kadhalika, mwonapo yamekwisha kuwa karibu. Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu. Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie. Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

Post a Comment

0 Comments