💜 Kijana yuko radhi avunje ratiba zake zote, ili akutane na mpenzi wake. Lakini hayuko tayari kwenda kanisani kukutana na Mungu wake, hata kama siku hiyo hayuko bize na majukumu yake.
💜 Kijana yuko radhi ayatoe maisha yake kwenye ujambazi na uuzaji wa madawa ya kulevya, ili apate pesa za haraka kwa ajili ya kumuhonga mpenzi wake. Lakini hayuko tayari kumtolea Mungu wake sadaka, akidai kuwa zinaliwa na Mapadre.
💜 Kijana yuko radhi aangalie mpira na tamthiliya mbalimbali za mapenzi usiku kucha, ili aiburudishe nafsi yake. Lakini hayuko tayari kuacha usingizi wake kwa ajili ya kumuomba Mungu ili roho yake ipate kuneemeshwa, kisa kesho asubuhi na mapema anawahi kazini.
💜 Kijana yuko radhi ashinde vijiweni na vibarazani, ili kusifia uzuri wa mpenzi wake na mambo mazuri anayomfanyia faraghani. Lakini hayuko tayari kujiunga na wenzake ndani ya chama chochote kile cha kitume, kwa ajili ya kuelimishana mambo ya Mungu.
💜 Kijana yuko radhi amalize bando lake, kwa ajili ya kuchati na mpenzi wake kila siku, hata kama maongezi yenyewe ni yale yale. Lakini hayuko tayari kutoa pesa yake, ili anunue Biblia kwa ajili ya kujifunza Neno la Mungu.
💜 Kijana yuko radhi apoteze muda kwa mambo ya starehe, huku akiwa na mpenzi wake. Lakini hayuko tayari kupoteza hata dakika moja, kwa ajili ya kusali na kumshukuru Mungu kwa uzima aliomjalia.
💜 Kijana yuko radhi kumnunulia mpenzi wake zawadi ya thamani sana, hata kama uwezo huo hana ili mradi tu amridhishe. Lakini hayuko tayari kuwapa watoto yatima zawadi yoyote ile hata kama kwake anaiona ndogo kiasi gani, ili azidi kubarikiwa.
💜 Kijana yuko radhi achangie mamilioni ya pesa, kwa ajili ya happy birthday ya mpenzi wake. Lakini hayuko tayari kulisaidia Kanisa kwa zaka, ili lipate kuendelea.
💜 Kijana yuko radhi kupost na kushare picha za mpenzi wake mitandaoni, hata kama zitaonekana hazifai kimaadili, ili apate followers, likes na comments nyingi. Lakini hayuko tayari kutuma wala kusambaza jumbe za Mungu, ili wengi wapate wokovu baada ya kuzisoma.
💜 Kijana yuko radhi kutoa maneno matamu kwa mpenzi wake, ili apate kumnasa. Lakini hayuko tayari kumsifu Mungu wala kumshuhudia kwa wengine, ili nao wapate kuonja upendo wa Mungu maishani mwao kupitia yeye.
💜 Kijana yuko radhi agombane na wazazi wake, kisa mpenzi wake. Lakini hayuko tayari kuchukiwa wala kutengwa na ndugu zake, kwa sababu ya kulipenda Kanisa na kulitumikia siku zote.
💜 Kijana yuko radhi kutembea barabarani na mpenzi wake, ili watu wapate kumsifia. Lakini hayuko tayari kubeba Biblia mikononi mwake, na kuanza kuwahubiriwa watu Neno la Mungu, kwa hofu ya kuchekwa na wapita njia.
💜 Kijana yuko radhi ampigie magoti mpenzi wake hata ikibidi kulia kwa machozi, hasa pale anapohisi amemkosea. Lakini hayuko tayari kumpigia Mungu wake magoti, ili kumwomba msamaha juu ya dhambi zake.
✝️ Hivyo kijana mwenzangu, kama na wewe ni miongoni mwa wale wanaowathamini sana wapenzi wao kuliko Mungu, basi naomba ubadilike sasa na umrudie Mungu kwa toba, kabla haijaja ile siku mbaya ya vilio na kusaga meno.
✝️ Kwani hata Yesu mwenyewe alipokufa Msalabani huku akiwa na miaka 33 tu, alikuwa na maana yake ya kutuonyesha thamani na njia nzuri ya kumtumikia Mungu katika umri huo wa ujana, kwa sababu bado tuna nguvu ya kumshinda shetani na kuleta mabadiliko chanya, ndani ya Kanisa na jamii yote inayotuzunguka. (1Yohane 2:13-14)
0 Comments