Ad Code

𝗝𝗘 𝗪𝗔𝗝𝗨𝗔 𝗞𝗪𝗔𝗡𝗜𝗡𝗜 𝗠𝗔𝗙𝗥𝗔𝗧𝗘𝗟𝗜 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗣𝗔𝗗𝗥𝗘 𝗛𝗨𝗩𝗔𝗔 𝗠𝗜𝗦𝗛𝗜𝗣𝗜 (𝗖𝗜𝗡𝗖𝗧𝗨𝗥𝗘)?

Ukweli ni kwamba, 𝗺𝘀𝗵𝗶𝗽𝗶 (𝘁𝗵𝗲 𝗰𝗶𝗻𝗰𝘁𝘂𝗿𝗲) ni mkanda uliotengenezwa kwa kitambaa maalumu, ambao huvaliwa kiunoni na Viongozi wote wa Kanisa Katoliki, kuanzia Mafrateli hadi Baba Mtakatifu.

Mishipi hii huonesha kifungo cha hiari kinachowekwa na Viongozi hao ya kuwa Watii na Waseja daima kulingana na nadhiri zao, kwa ajili ya kumtumikia Mungu tu na Kanisa lote kwa ujumla.

Hivyo anapovaa mshipi huo kiunoni, basi huashiria anajifunga na zinaa la kushiriki tendo la ndoa, na ndio maana huwa hawaoi. Na muda mwingine anapaswa kuwa Mtii kwa maagizo yote ya Kanisa, yatakayotolewa juu yake.

Pia mishipi hii huwa na rangi tofauti tofauti, mfano:

1. Nyeupe ➡️ Huvaliwa na Baba Mtakatifu.
2. Nyekundu ➡️ Huvaliwa na Makardinali.
3. Zambarau ➡️ Huvaliwa na Maaskofu.
4. Nyeusi ➡️ Huvaliwa na Mapadre pamoja na Mafrateli.

Lakini sio mishipi yote meupe, basi huvaliwa na Baba Mtakatifu peke yake. Kwani baadhi ya Mashirika hasa yale ya Kifransisko, Mapadre wao na Mfrateli wao (Brothers) huwa wanavaa mishipi ya rangi hiyo meupe.

Kadhalika pia mishipi hiyo mara nyingi huvaliwa baada ya Cassock, lakini kuna mshipi mwingine mwembamba unaovaliwa na Mapadre wote juu ya Alba kabla ya kuadhimisha Misa.
Mshipi huu humkumbusha Padre kuwa, licha ya kujizuia katika kuoa na kuwa mtii katika Kanisa, bado ana jukumu lingine la kubeba Msalaba wa Kristo katika utume wake, na ndio maana yuko tayari kuvumilia changamoto zozote zinazojitokeza dhidi yake. (1Petro 1:13)

𝗧𝗨𝗠𝗦𝗜𝗙𝗨 𝗬𝗘𝗦𝗨 𝗞𝗥𝗜𝗦𝗧𝗢...

Post a Comment

0 Comments