Ad Code

𝗠𝗭𝗔𝗭𝗜 𝗡𝗔 𝗞𝗔𝗡𝗜𝗦𝗔.

💜 Mzazi yuko radhi ampeleke mwanae shuleni, kwa ajili ya kupata elimu ya dunia. Lakini hayuko tayari kumpeleka mtoto wake kanisani, kwa ajili ya kujifunza mambo ya Mungu yatakayoimarisha imani yake.

💜 Mzazi yuko radhi atoe muda wake wote hata kama amebanwa na kazi, ili kumfundisha mwanae homeworks anazopewa shuleni. Lakini hayuko tayari kumfundisha mtoto wake sala mbalimbali za kanisa, kwa usalama wa roho yake.

💜 Mzazi yuko radhi mwanae ashinde shuleni nyakati zote, ili apate muda mzuri wa kujifunza masomo yake. Lakini hayuko tayari kumuona mtoto wake anakuwa kanisani zaidi ya saa moja, ili asije kufeli mitihani yake.

💜 Mzazi yuko radhi amnunulie mwanae madaftari na vitabu mbalimbali vya shuleni, ili ajifunze masomo yake kwa urahisi. Lakini hayuko tayari kumnunulia mtoto wake katekisimu wala chuo kidogo cha sala, ili ajifunze kwa uwepesi elimu yake ya dini.

💜 Mzazi yuko radhi akakope pesa mahali, ili amfanyie sherehe mwanae baada ya kuhitimu masomo yake. Lakini hayuko tayari kumfanyia mtoto wake sherehe ya komunyo ya kwanza wala kipaimara, kwa madai kuwa hana pesa za kuchezea.

💜 Mzazi yuko radhi akae sebuleni na mwanae, ili watazame filamu inayorushwa kwenye runinga. Lakini hayuko tayari kusali pamoja na mtoto wake sebuleni, kwa kisingizio kuwa ana kazi nyingi za kufanya.

💜 Mzazi yuko tayari kumuona mwanae akiwa na marafiki wanaopenda shule, ili wampe motisha ya kusoma zaidi. Lakini hayuko tayari kumuona mtoto wake akiambatana na marafiki wanaenda kanisani kila siku, kwa hofu kuwa atakosa muda wa kujisomea.

💜 Mzazi yuko radhi amuadhibu mwanae, pale anapofeli mitihani au kukataa kwenda shuleni. Lakini hayuko tayari kumchapa wala kumkemea mtoto wake, asipoenda kanisani kusali na wenzake.

💜 Mzazi yuko radhi kumfuatilia mwanae hata kwenda shuleni mwenyewe, ili kujua maendeleo yake ya kielimu. Lakini hayuko tayari pale anaporudi nyumbani kuwaulizia majirani zake, kama mtoto wake leo ameenda kanisani au la.

💜 Mzazi yuko radhi kumuona mwanae anakuwa daktari, mwalimu au askari pale anapomaliza shule. Lakini hayuko tayari kushauri wala kusikia mtoto wake anaenda utawani kuwa Padre, kwa hofu ya kukosa mwendelezo wa jina lake la ukoo.

✝️ Ukweli mzazi anaumia zaidi, pale anapomuona mwanae amefukuzwa shuleni kwa utovu wa nidhamu au kufeli mitihani yake, wakati amemgharamia kila kitu. Lakini hajali hata kidogo mtoto wake anapoacha kwenda kanisani, na kujiunga na makundi mabaya huko mitaani anakoishi.

✝️ Na ndio maana utakuta leo hii kanisani, wamejaa sana wazee kuliko watoto na vijana. Yote haya husababishwa na mzazi kushindwa kujua wajibu wake vema, katika kumlea mwanae kwenye maadili mema ya kanisa.

✝️ Hivyo tubadilike, kwani kanisa la kesho, mara nyingi hujengwa leo kwa malezi bora ya wazazi huko majumbani.

𝗧𝗨𝗠𝗦𝗜𝗙𝗨 𝗬𝗘𝗦𝗨 𝗞𝗥𝗜𝗦𝗧𝗢...

Post a Comment

0 Comments