Pale utu UNAPOKOMA mwanadamu hugeuka huwa kama mnyama.
Ile tunu ya kimungu iliyomo ndani yake hukoma.
Pale utu UNAPOKOMA hadhi ya kimungu iliyopi ndani ya mwanadamu hutoweka.
Pale utu UNAPOKOMA upendo hukoma na kulipa kisasi na mauaji hutamalaki.
Pale utu UNAPOKOMA mwanadamu si mwanadamu tena...si yule aliye umbwa Kwa sura na Mfano wa Mungu (ingawa ni yuleyule)....Hana tofauti tena na shetani! Aweza kuwa zaidi ya shetani.
Mwanadamu ameumbwa tofauti na Kwa namna ya pekee kuliko mnyama wa kawaida.
Yeye mwanadamu ameumbwa akiwa na akili pamoja na utashi.
Yaani akili na utashi vyote vifaidiane.
Akili itumike katika kujua na kuchanganua mema na mabaya...lakini utashi uamue kumshawishi mwanadamu kutenda au kutotenda kile ambacho akili imekichanganua na kufahamu!
Pale akili na utashi vinapokuwa hasi basi mwanadamu si mwanadamu tena...hugeuka na kuwa na tabia za wanyama kama si mnyama kabisa!
Mwanadamu,
Kila Kona ya dunia tunasikia mauaji....Kila Kona ya ulimwengu mwanadamu ana muua mwanadamu mwenzake.
Fikiria Nigeria watu waliuliwa wangali kanisani.
Fikiria vita vya Ukraine na Urusi watu wanauana.
Na sasa hata malangoni mwetu tunasikia habari za mauaji...inatisha na kutia hofu....hata hivyo Mungu anatuambia tumtumainie yeye...Anaendelea kusema Tusiogope wale wauao Mwili....Bali hasa yule mwenye uwezo wa kuua Mwili na Roho.
Tunaambiwa na Mathayo 10:28 BHN
Msiwaogope wale wauao mwili, lakini hawawezi kuiua roho.Afadhali zaidi kumwogopa yule awezaye kuuangamiza mwili pamoja na roho katika moto wa Jehanamu.
Lakini mioyo yetu ya kibinadamu imejaa woga na kukata tamaa...Ee Mungu tupe nguvu tuinuke tena.
Maisha ya mwanadamu yamekuwa kama mnyama ambaye anapelekwa machinjioni Kuchinjwa.
Yaani mtu haoni taabu kumuua mwenziwe Kwa sababu ya mamlaka.
Au cheo au kipande Cha ardhi.
Thamani ya maisha ya mtu haina maana tena...Ila kinachothaminiwa ni fedha...madaraka...ardhi na kutambuliwa katika jamii.
Tunasema kama Paulo katika waraka wake Kwa Warumi
Rum 8:36 SUV
Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.
Hata hivyo hatuchoki kuliitia jina la Bwana!
...........
Jamii yetu inapaswa kuelimishwa na kuihuisha tena ile roho ya utu.
Watoto wetu wasitazame sana filamu za mapigano ambazo zinachochea roho za mauaji na ukatili
Tuwafundishe wanetu kuhusu upendo na huruma ya Mungu, waweze kujaliana na kuhurumiana hata pale wanapokoseana
Watu Kila mtu Kwa nafasi yake atambue kuwa...Hana nafasi au mamlaka ya kutoa uhai wa mwingine
Tuzidi kuwafundisha watu wairudishe tena ile hofu ya Mungu iliyo jengeka mioyoni mwao
Tuishi maisha ya uadilifu na kupendana sisi Kwa sisi...Tukiikumbuka ile amri ya upendo aliyo tuachia Mungu Mkombozi wetu
Tuachane na dhana ya kulipiza kisasi...tujawe na msamaha Kila mara tunapokosewa
Kwa Mungu kuwe sifa na utukufu sasa na hata milele.
0 Comments