Ad Code

MASOMO YA MISA NOVEMBA 30, 2023 ALHAMISI, JUMA LA 34 LA MWAKA



SIKUKUU YA MT. ANDREA, MTUME

SOMO 1
Rum. 10:9-18

Ukimkiri Yesu kw akinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinyw ahukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika. Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.

Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema! Lakini si wote walioitii ile habari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, ni nani aliyeazimia habari zetu? Basi Imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Lakini nasema, Je! Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imeenea duniani mwote, na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.


WIMBO WA KATIKATI
Zab. 19:1-4 (K)

(K) Sauti yao imeenea duniani mwote.

Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu,
Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.
Mchana husemezana na mchana,
Usiku hutolea usiku maarifa. (K)

Hakuna lugha wala maneno,
Sauti yao haisikilikani.
Sauti yao imeenea duniani mwote,
Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu. (K)


SHANGILIO
Mt. 4:18

Aleluya, aleluya,
Bwana asema, Nifuateni, 
nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.
Aleluya.


INJILI
Mt. 4:18-22

Yesu alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.

Akaendelea mbele, akanona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohane nduguye, ambao walikuwamo chomboni pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita. Mara wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

Post a Comment

0 Comments