Ad Code

JE NI KWELI UTU WA KWELI UTAONEKANA WAKATI HUNA KITU?


Undugu, ndugu yako atakupenda na kufurahi pamoja kipindi cha mafanikio yako, utakula nae, utafurahi nawe kwenye nyakati zote si kwenye shida .

Wakati wewe umeishiwa atakuwa wakwanza kukusema, ulikuwa unaponda mali na kuzichezea hakumbuki mlikuwa mnaspend ote maisha.

Hapo ndipo utaona utu , maana ni wachache sana  baadhi ya hao ndugu zako,ndo watasimama nawe katika nyakati izo ngumu.


Marafiki nao ,hao watakuwa mstari wa mbele kukutenga , uliokuwa ukienda nao kwenye kumbi mbali mbali za starehe watakuita  umeishiwa.

Kwa ujumla kipindi wewe huna kitu ndicho kipindi muhimu cha kuchunguza na kuchuja yupi ni rafiki na yupi ni mnafiki.


Mpenzi wako, mchumba  wako, mkeo, mumeo, ukitaka upime upendo wa kweli ni kwenye nyakati wewe huna kitu,umefukuzwa kazi, biashara haina faida umefirisika ndo utamtambua upo na mpenzi kweli ama upo na nyang'au.

Kipindi umeishiwa mpenzi wako, mchumba wako na mkeo aliyekuwa anakupeti kwa maneno matamu hukaa mbali nawe kama ukoma , jua hana mapenzi ya dhati nawe ni mnafiki.


Kwa ujumla ,awe ndugu, mpenzi, mke , mume, rafiki wote hupimwa kwenye nyakati ngumu ndo utajua wangapi ni marafiki na wangapi walikuvisha kiremba cha ukoka maana nyakati hizi uongo na ukweli hujitenga mtu wangu.


▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬

Ushauri

Katika kutatua matatizo tunayokutana nayo kila siku, tunapaswa kutambua kuwa siyo kila tatizo lipo ili litatuliwe. Kuna baadhi ya matatizo yapo ili tuishi nayo kama changamoto zinazotuamsha na kutuchangamsha akili kila siku.


Katika uhusiano wako, jifunze kuishi na baadhi ya vipengele visivyokufurahisha katika mwenendo na maisha ya mwenzi wako. Vitu vingine vina mizizi mirefu sana katika hulka yake. Ninyi ni watu wawili tofauti wenye misimamo, historia na uzoefu tofauti. Ili kuwa na uhusiano wenye afya,ni vyema kutambua na kuridhia kuishi katika utofauti wenu.

Asantenii.!


Karibuni tena katika app ya Nyimbo za kikatoliki!!

Post a Comment

0 Comments