Ad Code

MFULULIZO WA MATUKIO KATIKA AJALI YA WANAKWAYA WA UVIKANJO MKOA WA NJOMBE

Watu wanane wamefariki dunia na wengine 19 wamejeruhiwa katika ajali ya gari (Coaster T 287 CCY) mali ya Kanisa Katoliki Njombe iliyogongana na lori la makaa ya mawe, RPC Njombe, Hamis Issah amethibitisha.


Watu hao ni miongoni mwa Vijana wanaounda Umoja wa Vijana Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe (UVIKANJO) ambao walikwenda kuwatembelea Watoto yatima katika kituo cha Ibumila Wilayani Njombe.


Ajali hiyo imetokea jana jioni katika eneo la Igima Wilayani Wanging’ombe Barabara kuu inayoelekea Mkoa wa Ruvuma.


RPC Issah amesema majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mji wa Njombe Kibena pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe.


TAZAMA VIDEOS ZIFUATAZO ZINAZOONESHA MATUKIO ZAIDI👇


Salamu za Raisi Samia

Rais Samia ametuma salamu za pole kwa wafiwa kutokana na vifo vya Watu 9 waliofariki kwa ajali ya gari Mkoani Njombe.


Akitoa salamu hizo kwa niaba ya Rais katika Ibada ya kuaga miili hiyo katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Jimbo Katoliki Njombe, RC wa Njombe, Waziri Kindamba, amewasihi Waombolezaji kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.


“Nichukue nafasi hii kutoa salamu za pole kutoka kwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye naye ameguswa sana na msiba huu”


Watu hao waliofariki ni miongoni mwa Vijana kutoka Umoja wa Vijana Kanisa Katoliki Njombe (UVIKANJO) na walifariki kwa ajali ya gari April 24,2022 katika eneo la Igima Kibaoni walipokuwa wakitoka kutembelea kituo cha kulea Watoto yatima kilichopo Ibumila Wilayani Njombe.

Raha ya milele uwape eeh Bwana......

Post a Comment

0 Comments